New Lyrics

Diamond Platnumz – Haunisumbui Lyrics

Diamond Platnumz - Haunisumbui Lyrics
Diamond Platnumz – Haunisumbui Lyrics

Diamond Platnumz – Haunisumbui Lyrics. (Ayolizer)

Si kokoko si kandambili
Yaani vyote havikupendezi
Mwana ngoko usio nawiri
Tope bin utelezi

Utaishia kututabiri
Tubomoke inasonga miezi
Mola ameshatakabiri
Usijichoshe halivunjiki penzi

Ona umekosa nuru
Umekosa bahati huna
Unaitwa kunguru
Ukifika wananuna

Ndo ndo ndo mwana chururu
Asiye mbuzi wataka chuna
Mengine nisikufuru mmmh

Hazikukai maskara
Wala make up zina kushuka
Uso ume ku parara
Mwili shock up zimetenguka

Uso sauti ya stara
Kwa kudeka una wehuka
Jibwa koko la Mbagala
Linabweka na kubwetuka wala

Wala haunisumbui wala
Wala haunisumbui wala
Wala haunisumbui wala
Wala haunisumbui wala

Na hizo post mara kubebana
Mara ati mnabusu mtamaliza bando
Unaowatuma ku nitukana
Siogopi mashushu me wala michambo

Kutwa kwa ma-page fake
Kama Lokole linahusu
Mkwe hakutaki eti
Mwenzangu pole mbona kuntu

Vi message kujitumisha
Kwa ndugu zangu marufuku
Nyota imekufubika
Usi-force umaarufu

Upepo wa kisulisuli
Unakuchukuwa na nuksali
Tanga lipulipuli
Wanakununua kwa mizani

Kwangu mpambe shughuli
Najiashua burudani
Na toto nzuri nzuri
Nimelitua tuli ndani ii

Ona umekosa nuru
Umekosa bahati huna
Unaitwa kunguru
Ukifika wananuna

Ndo ndo ndo mwana chururu
Asiye mbuzi wataka chuna
Mengine nisi kufuru
Usiye wa shaba wala chuma

Wala haunisumbui wala (Hamnikomeshi)
Wala haunisumbui wala (Mjipost ma Instagram)
Wala haunisumbui wala (Hamniteteshi)
Wala haunisumbui wala (Wala)

Dua Lipa Ft DaBaby – Levitating Lyrics

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button